Top Stories

Mtumishi wa Tazara afikishwa Mahakamani Kisutu DSM ‘Kesi ya Milioni 800’

on

Mfanyakazi Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Stewart  Mwangalaba (46) amepandishwa kizimbani kujibu shitaka la kujipatia zaidi ya Sh milioni 843 kwa njia ya udanganyifu. Mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Kibwegele Kibamba , Dar es Salaam alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Ruboroga.

Akisoma mashtaka, wakili wa serikali Eliya Atanas alidai shtaka la kwanza la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu analodaiwa kutenda kati ya Januari mosi mwaka 2017 hadi Oktoba 30 mwaka 2018 katika makao makuu ya Tazara. Ilidaiwa katika kipindi hicho, mshtakiwa alijipatia Sh 843,849,332 mali ya Tazara kwa kudanganya kwamba zinalipwa kwake kama fedha za safari na posho ya siku (perdm).

Katika shtakala pili, ilidaiwa katika tarehe na eneo hilo, mshtakiwa huyo alitakatisha kiasi hicho cha fedha wakati akijua ni mazalia ya kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Juni 16 mwaka huu.Mshtakiwa alirudishwa rumande na upande wa mashtaka ulidai mshtakiaa amepimaa hana maambukizi ya virusi vya Corona.

Soma na hizi

Tupia Comments