Top Stories

BREAKING: Aliekuwa Kamishna wa TRA Kitillya na wenzake wafutiwa kesi

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi ya utakatishaji fedha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamekamatwa tena kwa ajili ya kusomewa mashtaka mapya katika mahakama hiyo.

Kesi hiyo imefutwa mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mbando baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Hashim Ngole kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Ngole ameeleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo kwa kutumia kifungu cha 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mbando amesema anaiondoa kesi hiyo Mahakamani.

Hata hivyo, baada ya kutoa uamuzi huo washtakiwa waliweza kukamatwa na kupelekwa mahabusu ili wasomewe mashtaka mapya.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benk ya Stanbic Sioi Solomon.

Katika kesi ya awali, washtakiwa walikabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani Milion 6 katika akaunti tofauti tofauti  za benki ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015.

ZITTO NA WENZAKE WALIVYORUDI MAHAKAMANI MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA

Soma na hizi

Tupia Comments