Top Stories

BRELA yaongeza muda wa kuhakikisha taarifa za Makampuni

on

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya zoezi la uhuishaji wa taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (Online Registration System – ORS) hadi tarehe 31 Machi 2020.

BRELA inawataka wadau wote waliosajili Makampuni au Majina ya Biashara nje ya mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda ulioainishwa.

MAGUFULI ASHTUKIZA HOSPITAL ZANZIBAR AKUTA WATOTO WAKIWA HOI “MBONA HAWAHUDUMIWI”

Soma na hizi

Tupia Comments