Mechi za mwisho za hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya zinamalizika usiku wa December 8 na usiku wa December 9, tayari mechi za Kundi A, B, C na D zimemalizika, miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa December 8 ni mchezo kati ya Real Madrid ya Hispania dhidi ya klabu ya Malmoe FF.
Huu ndio mchezo ambao umemalizika kwa idadi kubwa ya magoli, Real Madrid ambao wanatajwa kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha wao Rafael Benitez, wameibuka na ushindi wa goli 8-0 dhidi ya klabu ya Malmoe FF, hivyo Real Madrid wamehitimisha hatua ya makundi kwa kuwa na jumla ya point 16 na kuongoza msimamo wa Kundi A.
Cristiano Ronaldo ndio alikuwa mchezaji hatari zaidi kwa Malmoe FF kwani alifanikiwa kufunga jumla ya goli 4, ambazo alifunga dakika ya 39,47,50 na 59 pamoja na kufanya assist mbili, Ronaldo alifunga goli hizo baada ya Karim Benzema kufunga goli 2 za awali dakika ya 12 na 24, baada ya hapo Mateo Kovacic akafunga goli la saba dakika ya 70 ila Karim Benzema akaja kumalizia goli la nane na la mwisho dakika ya 74.
Matokeo ya mechi za UEFA December 8
Kundi A
-
Paris Saint Germain 2 – 0 Shakhtar Donetsk
-
Real Madrid 8 – 0 Malmoe FF
Kundi B
-
PSV Eindhoven 2 – 1 CSKA Moscow
-
Wolfsburg 3 – 2 Manchester United
Kundi C
-
Benfica 1 – 2 Atletico Madrid
-
Galatasaray 1 – 1 FC Astana
Kundi D
-
Manchester City 4 – 2 Borussia Moenchengladbach
-
Sevilla 1 – 0 Juventus
Video ya magoli ya Real Madrid Vs Malmoe FF
https://youtu.be/WkzZJ64NoVU
Video ya magoli ya Wolfsburg VS Manchester United
https://youtu.be/7dcRtlO2Z7o
Video ya magoli ya Manchester City Vs Borussia Moenchengladbach
https://youtu.be/ghCktmmoHbM
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.