Ad
Ad

Michezo

Real Madrid wahitimisha mechi za makundi kwa kuichapa Malmoe, Cheki Full Time ya UEFA Dec 8 (+Pichaz&Video)

on

Mechi za mwisho za hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya zinamalizika usiku wa December 8 na usiku wa December 9, tayari mechi za Kundi A, B, C na D zimemalizika, miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa December 8 ni mchezo kati ya Real Madrid ya Hispania dhidi ya klabu ya Malmoe FF.

real-madrid-malmo-_3521568b

Takwimu za mchezo wa Real Madrid dhidi ya Malmoe FF

Huu ndio mchezo ambao umemalizika kwa idadi kubwa ya magoli, Real Madrid ambao wanatajwa kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha wao Rafael Benitez, wameibuka na ushindi wa goli 8-0 dhidi ya klabu ya Malmoe FF, hivyo Real Madrid wamehitimisha hatua ya makundi kwa kuwa na jumla ya point 16 na kuongoza msimamo wa Kundi A.

cl-qualified-teams_3521576b

Hizi ni baadhi ya timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora

Cristiano Ronaldo ndio alikuwa mchezaji hatari zaidi kwa Malmoe FF kwani alifanikiwa kufunga jumla ya goli 4, ambazo alifunga dakika ya 39,47,50 na 59 pamoja na kufanya assist mbili, Ronaldo alifunga goli hizo baada ya Karim Benzema kufunga goli 2 za awali dakika ya 12 na 24, baada ya hapo Mateo Kovacic akafunga goli la saba dakika ya 70  ila Karim Benzema akaja kumalizia goli la nane na la mwisho dakika ya 74.

Matokeo ya mechi za UEFA December 8

Kundi A

  • Paris Saint Germain 2 – 0 Shakhtar Donetsk
  • Real Madrid 8 – 0 Malmoe FF

Kundi B

  • PSV Eindhoven 2 – 1 CSKA Moscow
  • Wolfsburg 3 – 2 Manchester United

Kundi C

  • Benfica 1 – 2 Atletico Madrid
  • Galatasaray 1 – 1 FC Astana

Kundi D

  • Manchester City 4 – 2 Borussia Moenchengladbach
  • Sevilla 1 – 0 Juventus

Video ya magoli ya Real Madrid Vs Malmoe FF

https://youtu.be/WkzZJ64NoVU

Video ya magoli ya Wolfsburg VS Manchester United

https://youtu.be/7dcRtlO2Z7o

Video ya magoli ya Manchester City Vs Borussia Moenchengladbach

https://youtu.be/ghCktmmoHbM

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments