Serikali imewaagiza Viongozi wote wa Mikoa nchini kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki ya Vijana kujiajiri nasio kusubiria kuajiriwa ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya wiki ya vijana kitaifa yanayofanyika Mkoani Manyara katika Viwanja vya Stendi ya Zamani Mjini Babati.
Maadhimisho haya yanaenda sambamba na utunzaji wa mazingira kufuatia mabadiliko ya Tabianchi ambayo yameathiriwa na shughuli za kibinadamu Uzinduzi ambao umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi,Viongozi wa vyama na dini.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,vijana ,ajira na wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amewataka vijana na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Mkoani Manyara na Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Tiafa Ndugu Mohamed Kawaida akiiomba Serikali kurudisha Mikopo ya asilimia kumi ambayo ilikuwa ilitolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu kwa kuwa makundi hayo yanahitaji kushikwa mkono na Serikali