Imeelezwa kuwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Kitengo cha Saratani (Cancer) hupokea wagonjwa wapya 1,600 kila mwaka Hospitalini hapo kwa lengo ya kupata matibabu ya Saratani huku kundi la Wanawake likitajwa kuongoza.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani Hospitali ya Bugando Dkt. Nestory Masalau anasema magonjwa ya Saratani bado ni tatizo kwa ukanda wa ziwa kwani hupokea wagonjwa wengi wakiwemo wanawake.
Katika kurahisisha utoaji wa huduma kwa kitengo hicho taasisi isiyo ya Kiserikali ya JEMA imefika imekabidhi vifaa tiba vitakavyosaidia utoaji wa huduma kwa Wagonjwa wa Saratani.
Bi. Jema Baruani ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Jema Foundation ambae ni muhanga wa ugonjwa wa Saratani kwa miaka 7, anawahasa wagonjwa wa Saratani kutokimbilia kwa waganga wa jadi na badala yake wawahi Hospitali kwa matibabu.