Ikiwa leo ni siku ya himofilia duniani Hospitali ya Taifa Muhimbili imezindua rasmi maabara maalum yenye mashine za vipimo vya ugonjwa huo kwa ajili ya wagonjwa wa tatizo hilo kuhakikisha wanapatiwa matibabu katika hospitali hiyo na hospitali zote za kanda ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Takribani watu 200 nchini wanakadiriwa kuwa na tatizo la ugonjwa wa himofilia ambao ni ukosefu wa chembechembe za protini zinazosaidia damu kuganda mwilini pale mtu anapopata ajali au kutokwa damu sehemu yoyote ya mwili wake.
Kutokana na uzito wa tatizo hilo hospitali ya Taifa Muhimbili ikaja na mpango wa kutekeleza jukumu la kufanya matibabu kwa wagonjwa hao, jambo ambalo linaungwa mkono na Mganga mkuu wa serikali Prof. TUMAINI NAGU.
Dkt Stella Rwezaura ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya damu katika hospitali ya Taifa Muhimbili ameeleza namna ambavyo mashine zilizozinduliwa zitakavyofanya kazi.