Habari za Mastaa

Muhimbili yalaani video ya Prof. Jay akiwa ICU ‘Hatujarekodi sisi’

on

Hospitali ya Taifa Muhimbili imetolea ufafanuzi taarifa inayosambaa kwenye mtandao wa kijamii kuhusu Joseph Haule Joseph Haule maarufu Prof. Jay.
 “Kuna video inayosambazwa na Mtandao wa Mange Kimambi ikimuonesha Profesa Jay akipatiwa matibabu Muhimbili Hospitali Upanga”

“Uongozi wa Hospitali unatoa taarifa kuwa video hii haijarekodiwa na kusambazwa na Hospitali, tumesikitishwa na tunalaani vikali kitendo hiki cha kumrekodi mgonjwa anayepigania uhai wake ICU na kuisambaza, hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu na maadili”- Muhimbili

“Tunafuatilia kwa ukaribu tukio hili ili kubaini chanzo cha video hiyo ili hatua stahiki zichukuliwe, Wananchi endeleeni kuwa na imani na Hospitali ta Muhimbili” imeeleza taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Muhimbili’- Muhimbili

 

 

ASKARI ALIYEJICHIMBIA KABURI AMBAYE NI BABA WA TUNDA AFUNGUKA KUHUSU WHOZU ‘NDOA LAZIMA IFUNGWE’

Tupia Comments