Muigizaji wa nguli na wazamaani kabisa Uswidi Dolph Lundgren, 65 maarufu kwa watoto wa zamni wakimwita Adolfu ambaye ameigiza katika filamu nyingi, kama vile filamu ya Rocky IV, amefunguka katika mfululizo wa filamu za hivi majuzi jinsi amekuwa akipambana na saratani ya mapafu kwa miaka nane sasa
Muigizaji huyo aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu kwa mara ya kwanza mnamo 2015 anasema alipata nafuu lakini saratani ikarejea mwaka wa 2020, na akaambiwa alikuwa amebakiza miaka 2-3 kuishi na daktari mmoja.
Muigizaji huyo wa Uswidi alifunguka kuhusu pambano lake la ‘In Depth with Graham Besinger’ na akafichua kuwa aligunduliwa na saratani ya mapafu kwa mara ya kwanza mwaka wa 2015.
Katika kipande cha picha ya mahojiano hayo, akiwa bado amevalia vazi la hospitali, anasema: ‘Ni siku moja baada ya upasuaji wangu, walitoa uvimbe mmoja, kisha wakatoa nyingine mbili wakapata na nyingine tatu ndogo.
‘Natumai imesafishwa, ikifa, inakufa.’
Lundgren alikuwa akirejelea nukuu yake ya kukumbukwa katika filamu ya Rocky IV ya 1985, baada ya mhusika wake Ivan Drago kumuua Apollo Creed wakati wa mechi yao ya maonyesho.
‘Waligundua kuwa kulikuwa na vivimbe zaidi kuzunguka eneo hilo.’
“Wakati huo ilianza kunigusa kwamba hii ilikuwa ni jambo zito. Daktari wa upasuaji aliniita na kusema kuwa ni kubwa, ni kubwa sana, ilikua na ukubwa wa limao ndogo.
Nikawauliza nimebakiza muda gani, nadhani alisema miaka 2-3 lakini niliweza kusema kwa sauti yake alidhani ni kidogo. Nilidhani hiyo ndiyo hakika.’
Lundgren alisema kuwa matumizi ya steroids yalikuwa na athari kwenye mwili wake