Top Stories

Mume ajinyonga baada ya kuachwa na mkewe

on

Mkazi wa Kijii cha Ng’wandakw, Kata ya Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Philemon Tandu (50) amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kuachwa na mke wake akiwa na watoto watano.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Kamishna msaidizi (ACP) Marrison Mwakyoma akizungumza amesema tukio hilo lilitokea juzi kwenye kijiji hicho cha Ng’wandakw.

Kamanda Mwakyoma amesema marehemu huyo, Tandu (50) alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani shingoni baada ya mkewe Christina Elia (45) kumuacha akiwa na watoto watano.

Amesema chanzo cha kifo hicho ni matatizo ya familia ambapo mara baada ya Tandu kuachwa na mkewe alichukua uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani.

Amesema baada ya mwanamke huyo kutaka kumwacha mumewe walijaribu kusuluhisha ugomvi wao ili wasiachane na walee watoto wao ila ikashindikana mwanamke huyo akaondoka.

“Tandu alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani karibu na nyumba yake mara ya mkewe kuondoka nyumbani kwao akidai hamtaki tena na kumwachia watoto watano,”  Kamanda Mwakyoma.

MESSI ASHINDWA JIZUIA AMWAGA MACHOZI MBELE YA WACHEZAJI WENZIE

 

Soma na hizi

Tupia Comments