Habari za Mastaa

Kwa unaefatilia maisha ya mastaa, Snura atavaa vya aina hii sana 2014,

on

IMG-20140102-WA0039Miongoni mwa wasanii wa Bongo fleva ambao hawatoweza kuusahau mwaka 2013 pengine Snura nae yupo kwenye list na hii ni baada ya meneja anayesimamia kazi zake za muziki Hemed Kavu au HK kuzungumza na millardayo.com na kuelezea mafanikio yote ya mwaka 2013 aliyoyapata staa huyu mwa ‘Majanga

IMG-20140102-WA0033Hk anaanza lwa kusema>>>Kiukweli mwaka 2013 tulifanya vitu vingi vikubwa kwa sababu naamini msanii wangu ni msanii pekee wa kike aliyefanya show nyingi hata kwa wanaume hakuna anayemfikia Snura,kuna show tunafanya hadi j’4.j’5 hadi alhamisi tumekua tukizifanya show hizo.

‘Kwa ujumla kuhusu pesa tulizoingiza kwa mwaka 2013 ni mpunga mrefu kwa sababu tumefanya show zisizopungua 180 kwa mfano tunapiga Njombe,tunapiga Songea,tunapiga na Mbinga so kwa wiki tuna uhakika kwa wiki tunafanya show zisizopungua 4 hadi 5

‘Ngoma ya Majanga imehit mwez wa 3 ndo tukaanza kukamata show lakini kabla ya hapo tulikua na nyimbo ya shogaake mama na debe la vanga na tulikua tunafanya show pia,tuna jumla ya show kama 20 za makampuni na hizi ni zile tunalipwa milion 3 hadi milion 4.

‘Kwa siku tunaweza kupiga show hadi 3 kwa mfano kuna siku tulikua na show Z’bar tukaja Dar kulikua na show ya kampuni pale Amana,tukatoka hapo tukawa na show mchana huo huo na usiku tukapiga tena show,Mpunga ni mrefu ni zaidi ya Milion 100’.

‘Kuna dili tulikua tumepata ya Snura kuwa balozi wa kampuni fulani lakini mkataba ndo tunaweza kusaini mwezi huu a,mbao utakua ukihusisha pia na show kwa Snura ambapo watatoa shows 30 ambazo kila show moja tutakua tukifanya kwa milioni 7 kwa hiyo kuna Milion 210 zipo’.

‘Kwa Snura mwaka 2014 amekuja na mavazi yake ambayo tumebuni wenyewe kwa hiyo kuna style mpya ya mavazi na moja kati ya wasanii wanaovaa nguo za heshima ni pamoja na Snura japo mwili wake ndo una tetemesha lakini ndo kaumbwa hivyo inabidi tukubali’.Hk.

 

 

Tupia Comments