Duniani

Kumbe Rais Museveni alimsalimia Rais Obama kwa mkono wa kushoto, kuna tatizo? (+Video)

on

Kuna ishu ya baadhi ya watu kutumia mikono ya kushoto kuandika badala ya mkono wa kulia kama ambavyo imezoeleka, hiyo sio story ya kushangaza, lakini ni kawaida watu kusalimiana kwa mikono ya kulia, ikitokea mtu anakusalimia kwa mkono wa kushoto unaweza usiichukulie poa..

Rais Museveni kamsalimia Rais wa Marekani, Barack Obama kwa mkono wa kushoto walipokutana kwenye Mkutano wa Marais Marekani.. sio kila mtu alielewa sababu hasa, Rais Obama alimtania wakati huohuo Museveni >>> ‘Kuna mtu mlisumbuana nini ukampiga ngumi?‘.. Rais Museveni akajibu >>> ‘Hapana, ilikuwa ni ajali tu‘>>>

musevenideclaredpix

Ukweli ni kwamba Rais Museveni alikuwa na bandage mkononi, Taarifa kutoka Ikulu ya Uganda ilitolea ufafanuzi kuhusu ishu ya Rais wao kuwa na bandage mkononi ambapo wamesema Rais Museveni alijigonga kwenye mlango wa gari wakati akiwa anaharakisha kuwahi safari yake kwenda Japan.

Wapo waliohisi kwamba msimamo wa Rais Museveni kuhusu ishu ya Ndoa na uhusiano wa jinsia moja imefanya amsalimie kwa mkono huo Rais Obama, kitu ambacho Ikulu ya Uganda imekanusha kwamba hakuna uhusiano wowote kwenye hayo mawili.

Kipande cha video hiki hapa pamoja na stori za Rais Obama na Rais Museveni uso kwa uso…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments