Bilionea na mmiliki wa jukwaa la X Elon Musk ameanzisha hatua za kisheria dhidi ya msururu wa makampuni baada ya kuacha kutangaza kwenye mtandao wake wa kijamii.
Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, inadai kuwa kampuni hizo zilipanga njama isivyo halali kususia tovuti hiyo na kuisababishia hasara ya “mabilioni ya dola” katika mapato.
Musk amekuwa akikosolewa zaidi juu ya uendeshaji wake wa X ambayo hivi majuzi imelaumiwa kwa kushindwa kushughulikia habari potofu zilizoenea wakati wa ghasia nchini Uingereza.
Kesi hiyo iliwasilishwa Texas dhidi ya Shirikisho la Dunia la Watangazaji na makampuni wanachama wa Unilever ya kimataifa ya Uingereza, kampuni kubwa ya chakula ya Mars, CVS Health na kampuni ya nishati mbadala ya Denmark ya Orsted
Kesi hiyo inadai makampuni hayo wanaofanya kazi kupitia mpango wa Shirikisho la Dunia la Watangazaji uitwao Global Alliance for Responsible Media (GARM) – walishirikiana kwa njia ambayo ilikiuka sheria za Marekani za kuondoa uaminifu kwake.
Mpango huo ulizinduliwa mnamo 2019 ili “kusaidia tasnia kushughulikia changamoto ya maudhui haramu au hatari kwenye mifumo ya media ya dijiti na uchumaji wake wa mapato kupitia utangazaji”.
Musk aliandika kwenye X: “Tulijaribu amani kwa miaka miwili, sasa ni vita.”
Inakuja baada ya mapato ya utangazaji katika X kupungua baada ya Musk kununua na kubadilisha jina la mtandao wa kijamii kwa $44bn (£35bn) mnamo 2022.