Tume ya Usalama na Masoko ya Marekani (SEC) imemshtaki bilionea Elon Musk kwa kutofichua kwa wakati ununuzi wake wa asilimia 5 ya hisa za Twitter (sasa X) mnamo 2022 kabla ya kununua kabisa kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii.
Musk tajiri zaidi duniani alinunua hisa mnamo Machi 2022 na malalamiko ya Tume ya Usalama na Ubadilishanaji ya Marekani (SEC) yalisema kuchelewa kulimruhusu kuendelea kununua hisa za Twitter kwa bei ya chini.
HIvi sasa tume hiyo inamtaka Bw Musk alipe faini ya kiraia na kurudisha faida ambayo hakustahili kupata.
Kitendo cha leo ni kukiri kwa SEC kwamba hawawezi kuleta kesi halisi – kwa sababu Bw. Musk hajafanya chochote kibaya, na kila mtu anaona udanganyifu huu kwa jinsi ulivyo,” wakili wa Musk, Alex Spiro, alisema katika taarifa ya vyombo vya habari.
Sheria ya SEC inahitaji wawekezaji kufichua ndani ya siku 10 za kalenda wanapovuka kiwango cha umiliki cha 5%.
SEC ilisema Bw Musk hakufichua chochote yake tarehe 4 Aprili 2022, siku 11 baada ya tarehe ya mwisho – ambapo alikuwa anamiliki zaidi ya 9% ya hisa za Twitter.