Kutoka Bungeni Dodoma leo September 22, 2022 unafanyika uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambapo wagombea wamepata nafasi ya kujieleza mbele ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alipokuwa akiomba kura Mohamed Habib Mnyaa, mmoja wa wabunge walioibua shangwe ni Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma baada ya kusimama na kuuliza swali kwa lugha ya kiingereza.