Top Stories

Muuguzi ajiua baada ya kupata Corona

on

Muuguzi wa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya San Gerardo, Daniela Trezzi (34) amejiua baada ya kupata maambukizi ya COVID19 na kuhofia kuwa atawaambukiza wengine.

Mbali na hofu ya kueneza Virusi hivyo, imeelezwa kuwa Daniela pia alikuwa na msongo wa mawazo uliosababishwa na kazi kubwa wanayofanya watumishi wa afya katika kudhibiti Corona Virus.

Kabla ya kifo chake aliwaambia wafanyakazi wenzake kuwa ana wasiwasi amemuambukiza mtu mwingine Virusi hivyo.

Uchunguzi zaidi wa kifo cha Daniela Trezzi unaendelea.

BREAKING: MBOWE ATHIBITISHA MTOTO WAKE WA KWANZA KUPATA CORONA, “HILI NI JANGA KUBWA”

Soma na hizi

Tupia Comments