Muuguzi katika hospitali ya New York amesimamishwa kazi na sasa anachunguzwa na polisi baada ya baba kuchukua kipande cha video wakati mtoto wake mchanga akipigwa kofi la usoni na muuguzi huyo alipokuwa akimhudumia.
Tukio hilo lilitokea katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Good Samaritan huko West Islip huku tarehe ya tukio hilo haikufahamika mara moja.
Polisi wa Suffolk walisema katika upelelezi na ripoti ni kuwa mtoto huyo, Nikko, alikuwa na umri wa siku mbili pekee alipokuwa akipatiwa matibabu na dawa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali ya Neonatal ndipo baba wa mtoto huyo mchanga, Fidel Sinclair, alipoanza kurekodi video ya mtoto wake kupitia mapazia ambayo hayakuonyesha tukio hilo vizuri.
Video kisha ilinasa muuguzi anayedaiwa kumgeuza kwa nguvu mtoto kutoka mgongoni na kumgeuzia upande wa tumboni kwenye sehemu aliyowekwa
Sinclair aliliambia shirika moja la habari kuhusu tukio hilo na kusema;
“Nimefurahi kuwa pale huenda Mungu alinituma,”
“Kama si Mungu, … tusingewahi kuona lolote kati ya hayo likitokea na huenda hilo lingeendelea kutokea usiku kucha, si kwake tu, bali kwa watoto wengine pia.”
“Kwa kuwa huu ni uchunguzi wa wazi, Idara haiwezi kutoa maoni zaidi malalamiko yote ya hospitali huwekwa kuwa siri na uchunguzi utakapokamilika matokeo yanashirikishwa kwa umma,” ilisema taarifa kutoka idara ya afya ya serikali.