AyoTV

Waziri Mwijage kuhusu mvinyo unavyoweza kukulinda na magonjwa

on

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kinywaji kipya cha mvinyo kilichopewa jina la IMAGE ambacho kitakuwa kikitolewa katika ndege za ATCL zinazomilikiwa na serikali ya Tanzania ambapo amewataka Watanzania kuweka uzalendo wa kunywa kinywaji cha mvinyo inachozalishwa nchini kutokana na zao la zabibu huku akieleza namna matumizi ya kinywaji hicho kinavyoweza kumkinga mtu na baadhi ya magonjwa mwilini.

Ninafurahi namna AirTanzania mlivyoamua kuja na mtazamo mpya wa kuitangaza bidhaa ya watanzania, kitendo cha kuamua huu mvinyo kunyweka ndani ya ndege ni imani yangu kubwa hatua hii itawashawishi watu wengi kupendelea kunywa mvinyo huu” –Waziri Mwijage

Tunaambiwa kwamba mvinyo ni chakula kinachotibu na kuna mtaalamu alishasema usipokula chakula cha lishe basi utakuja kula dawa kama chakula” –Waziri Mwijage

Full video nimekuwekea hapa chini tayari….

Waziri Jafo baada ya kukuta wananchi wamechanga Milioni 26 kujenga kituo cha afya

Soma na hizi

Tupia Comments