Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema mvua za El Nino zinazokaribia kunyesha huenda zikawa na athari hasi kwa watu milioni 1.2 nchini Somalia mwaka huu.
Shirika hilo limesema katika mpango wake wa hivi karibuni uliotolewa mjini Mogadishu kuhusu kupunguza, maandalizi na majibu kwa mwezi Agosti 2023 hadi Januari 2024, kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa ili kulinda uhai na maisha ya watu.
Kwa mujibu wa Shirika hilo, jamii zinazoishi kando ya mito ziko hatarini zaidi huku hekta karibu milioni 1.5 za ardhi zikiwa katika hatari ya kukumbwa na mafuriko, na kuongeza kuwa hatua za awali zinaweza kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.
Mbali na hatari halisi za kibinadamu, FAO ilisema mvua kubwa inayotarajiwa inaweza kupatikana ili kusaidia kuimarisha uzalishaji wa kilimo na kurejesha maisha.
“Kwa msaada na taarifa kwa wakati, jamii za vijijini katika maeneo ya mvua na mito inaweza kujaza vyanzo vya maji na kuimarisha usalama wa chakula kufuatia misimu mitano mfululizo ya mvua duni,” FAO ilisema.
Kulingana na FAO, itasaidia ufufuaji wa maisha na kulinda rasilimali za uzalishaji ikiwa ni pamoja na kilimo cha mdororo wa uchumi, uhawilishaji wa fedha unaotegemea utabiri pamoja na afua za kudhibiti wadudu na matibabu ya mifugo.