Mchezo wa mfululizo wa ligi kuu ya Italia kati ya mahasimu AS Roma na Parma umeahirishwa baada ya dakika 8 za mchezo baada ya mvua kubwa kunyesha na kufanya kuighalishwa kwa mchezo huo.
Kulikuwa na shaka kuhusu mchezo huo uliofanyika katika dimba la Rome Stadio Olimpico kama ungefanyika kabisa jumapili ya leo kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika mji mkuu wa Italia hali iliyopelekea kuchelewa kuanza kwa mchezo huo.
Ni dakika nane tu zilitumika uwanjani kughairisha mchezo huo kabla ya refa kuamua kuisimamisha mechi hiyo kwa dakika 30, akiruhusu kufanyika kwa ukaguzi wa uwanja ili kuona kama inafaa kuendelea kwa mchezo huo, lakini mechi hiyo ikabidi kuhairishwa kufuatia ukaguzi kuonyesha haitofaa mchezo huo kuendelea.
Haijapangwa tarehe mpya ya kurudiwa kwa mchezo huo na ni vigumu kesho Jumatatu kwa sababu Roma wanaikaribisha Napoli katika nusu fainali ya Coppa Italia siku ya Jumatano.