AyoTV

VIDEO: Wasamaria walivyomfuta machozi Mwanafunzi wa UDSM aliyelia gazetini kwa kukosa mkopo

on

Alionekana kwenye Magazeti likiwemo la Mwananchi akitokwa machozi na kujifuta baada ya kuona jina lake halipo kwenye orodha ya waliopata mkopo chuo kikuu cha Dar es salaam, jina lake ni Edson Mwakyombe ambaye alifaulu Form VI kwa Dividion 1.8

Baada ya Wasamaria kumuona kwenye gazeti, kupitia kwa Mwanasheria Albert Msando wakaomba kukutana nae tayari wakiwa wameguswa kumsaidia malipo na wakafanikiwa kulitimiza hilo November 1 2016.

Kiufupi ni kwamba Wasamaria wawili Isaria Mlaki na Andrew Komba waliojitokeza kumsaidia wamemuahidi kumsomesha kwa miaka miwili kila mmoja akimsomesha kwa mwaka mmoja.

Baada ya hayo Edson mwenyewe amesema ‘Nashukuru kwamba jambo hili limewagusa watu, naiomba serikali matatizo kama haya ya mkopo wayaangalie sana kwani kuna baadhi ya watu pia wanateseka sana huku chuoni kwetu, pia ninawaahidi hawa waliojitokeza kuwa nitahakikisha nafanya vizuri katika masomo yangu

.

Edson Mwakyombe akiwa na msamaria wake Isaria Mlaki aliyejitolea kumsomesha mwaka wa pili chuoni

.

Andrew Komba ambae ambae amejitolea kumsomesha masomo yake ya mwaka wa kwanza, Edson katikati na Mwanasheria Albert Msando

UNAWEZA KUMTAZAMA EDSON KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI AKIONGEA..

ULIPITWA NA KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU WANAFUNZI WALIOKOSA MKOPO? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

ULIYAKOSA MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2016? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI MWANZO MWISHO MPAKA MSHINDI ALIVYOPATIKANA

Soma na hizi

Tupia Comments