Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Urembo Duania ( Miss World), Miss Tanzania Halima Kopwe @halimakopwe amerejea nchini siku ya leo akitokea nchini India ambako lilikuwa likifanyika shindano hilo huku akiwa na mafanikio ya kuingia kwenye orodha ya Warembo 40 bora waliowania taji la Miss World 2024 kwenye mchujo ambao umewaacha nje Warembo wengine 72 kutoka kwenye idadi ya jumla ya Washiriki 112.
Halima amefika na kupokelewa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa waliomuwakilisha Katibu wa Baraza hilo na alipofika amefunguka kujivunia kuiwakilisha Tanzania Kwenye hatua Mbali Mbali ikiwemo hiyo ya kuingia Nusu fainali yenye top 40
Mara ya mwisho mshiriki wa Tanzania kuingia 40 Bora ilikuwa ni mwaka 2005 ambayo alifanikiwa kuingia Nancy Sumary, pia Halima amefanikiwa kuingia top 10 ya Project bora Duniani kupitia Kampeni yake ‘My Blood My Generation’