Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, amewataka Watanzania kuwa na subra kwani uchunguzi wa tukio la vifo vya watu 20, vilivyotokea Mjini Moshi, bado unaendelea, licha ya Mtume Mwamposa pamoja na wenzake saba kuachiwa kwa dhamana.
Katika taarifa yake leo ACP Misime, amesema kuwa, Mtume Mwamposa pamoja na wenzake wameachiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria na kwamba uchunguzi utakapokamilika Watanzania watajulishwa.
“Katika uchunguzi huo walikamatwa watu Nane akiwepo Mwamposa na kuhojiwa kwa kina na baada ya kujiridhisha na yale yaliyokuwa yanahitajika kutoka kwao, wamepewa dhamana kwa mujibu wa sheria ili waendelee kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea na ukikamilika yatakayobainika yatatolewa kwa mamlaka husika na kutekelezwa” ACP Misime.
WAITARA AZOMEWA NA WAPINZANI BUNGENI, ISHU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA