Habari za Mastaa

Mwana FA kaeleza anavyoendelea kiafya baada ya kukutwa na Corona Virus

on

Staa Mkongwe kwenye game ya Bongofleva Mwana FA amewashukuru waliomtumia salam za pole na kuelezea hali yake ya kiafya inavyoendelea toka alipogundulika kuwa amepata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwana FA amendika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa..>>>”Nawashukuru kwa salamu za pole na dua ndugu zangu. Kama nilivyosema,sijisikii kuumwa tena hata,KABISA. Hata ile homa iliyonipa wasiwasi nikaenda kupima haijarudi toka jana.Malaria ina tabu zaidi ya kaugonjwa haka nawaambia. Asikutishe mtu.” Mwana FA

TAZAMA HAPA MWANA FA ALIVYOTHIBITISHA KUKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA

 

Soma na hizi

Tupia Comments