Pamoja na kumiliki Newcastle United, Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia [PIF] pia umezindua LIV Golf na kuwekeza mamilioni katika Ligi ya Saudi Pro, ambapo wanamiliki timu nne – ikiwa ni pamoja na Al Nassr ya Cristiano Ronaldo.
Taifa hilo la Mashariki ya Kati limeshutumiwa kwa kutumia michezo kuboresha sifa yake huku kukiwa na ukosoaji na wasiwasi juu ya ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kunyongwa kwa wanaume 81 katika siku moja mwaka jana, masuala ya haki za wanawake na kuharamisha ushoga.
Lakini akizungumza na Fox News, Bin Salman alisema: “Ikiwa unawaji wa michezo utaongeza Pato la Taifa langu kwa asilimia 1, basi tutaendelea kuosha michezo.
“Sijali kuhusu maneno yoyote,nina ukuaji wa asilimia 1 katika Pato la Taifa kutokana na michezo na ninalenga asilimia 1.5 nyingine.
“Iite unavyotaka – tutapata hiyo asilimia 1.5.”