Michezo

Mwanamke alivyosababisha Messi kumfukuzisha Icardi “alioa Mke wa mchezaji mwenzie”

on

Lionel Messi ametua PSG kama mchezaji huru lakini wengi wanajiuliza vipi itakuwaje maisha ya Lionel Messi na Mauro Icardi ndani ya kikosi hiko, wote hao ni rai wa Argentina na wamekuwa wakiitumikia timu yao ya Taifa.

Mara kadhaa imeripotiwa kuwa Messi na Icardi hawapikiki chungu kimoja hii inatokana na Icardi kumuoa mke wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Sampdoria anayejulikana kwa jina la Maxi Lopez huyu ni Muargentina na rafiki wa Lionel Messi.

Inadaiwa kuwa Mauro Icardi alikuwa chanzo cha mifarakano kati ya Maxi Lopez na aliyekuwa mkewe Wanda Nara kiasi cha kuachana wawili, baada ya kuachana Icardi akautumia mwanya huo na kufunga ndoa na Wanda Nara na sasa wana watoto.

Kitendo hiko hakikumpendeza Messi hata kidogo na kumuona Icardi kama msaliti kiasi cha kudaiwa Messi 2018 katika kikosi cha Kombe la Dunia alimshinikiza kocha wao Argentina wakati huo Jorge Sampaoli asimuite timu ya taifa Mauro Icardi.

Taarifa za kutokuwa na maelewano kati ya Icardi na Messi, Icardi amewahi kuzikanusha na kusema wapo sawa japokuwa vyanzo vya vinadai mambo sio mazuri sana, sasa hivi kuna taarifa kuwa Club ya PSG inataka kufanya mabadilishano na Atletico Madrid wamtoe Icardi na wao wapewe Luis Suarez taarifa ambazo zinapigilia msumari wa tetesi kuwa Messi bado hayuko sawa na Icardi.

MWANAMKE ALIVYOSABABISHA MESSI KUMFUKUZISHA ICARDI “ALIOA MKE WA MCHEZAJI MWENZIE”

Soma na hizi

Tupia Comments