Majeshi ya Israel yamemuokoa mwanamke mmoja raia wa Iraq aliyetekwa nyara miaka 10 iliyopita na watu wanaojiita Islamic State kabla ya kushikiliwa mateka huko Gaza.
Fawzia Amin Sido, 21, alirejea Iraq siku ya Jumatano, mamlaka ya Iraq ilisema.
Jeshi la Israel lilisema Alhamisi kwamba mwanamke huyo aliachiliwa katika operesheni ya uokoaji mapema wiki hii ambayo iliratibiwa na Marekani.
Wanamgambo wa Islamic State walifanya utumwa na kuua maelfu ya watu wachache wa dini ya Yazidi walipoteka maeneo mengi ya kaskazini mwa Iraq na mashariki mwa Syria mwaka wa 2014.
Kwa mujibu wa jeshi la Israel, Bi Sido alitekwa nyara na IS alipokuwa na umri wa miaka 11 na wakati fulani alisafirishwa hadi kwa Mpalestina na kuletwa Gaza.
Jeshi lilisema kuwa Mpalestina huyo ni wa Hamas na aliuawa, kwa shambulio la anga. Msemaji alisema Bi Sido alichukuliwa kupitia mpaka wa Kerem Shalom, unaounganisha Gaza na Israel. Kutoka huko alisafiri hadi Jordan na kisha Iraqi, ambako aliunganishwa tena na wanafamilia.