Top Stories

Mwanamke amuua Mumewe ‘Kisa aliulizwa kwanini amechelewa kurudi nyumbani’

on

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia mwanamke aitwaye Riziki Henry (22), Mkazi wa Nditu wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za mauji ya mume wake Ayubu Aron(33) ambaye alimuua kwa kumpiga na kitu butu kichwani kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali kisogoni baada ya kuulizwa sababu za  kuchelewa kurudi nyumbani usiku.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema  tukio hilo la mauji lilitokea April 2 majira ya saa tisa alasiri mwaka  huu huko katika kijiji cha Nditu ambapo mtuhumiwa baada ya mume wake kuchelewa kurudi nyumbani usiku kulitokea ugomvi ulisababisha mauaji.

Matei amesema baada ya tukio hilo, Aron alikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Rungwe (Makandana) kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini April 2 mwaka huu majira ya saa 11 jioni alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.

Tupia Comments