Zuwena Msonyo ni mkazi wa kijiji cha Nanguruwe kata ya Nanguruwe Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara ambaye amejiajiri katika biashara ya kuuza mkaa kwa kutumia baiskeli kitu ambacho sio cha kawaida hasa kwa Mwanamke kufanya biashara hiyo kutokana na ugumu wa kazi hiyo.
Zuwena anakwenda mwenyewe porini na kufuata hatua zote za namna ya kuupata mkaa huo ikiwa ni pamoja na kuutoa mkaa huo kwenye tanuru lenye moto, kuupoza, kuujaza kwenye viroba, kuupakiza kwenye baiskeli na kisha kwenda Mtwara mjini kuuza na kazi hizo anazifanya pekee yake.
Zuwena amesema sababu iliyomfanya ajiingize kwenye biashara hiyo mapema mwaka huu ni hali ngumu ya maisha na ana Watoto wawili anaowasomesha kupitia biashara hiyo, haoni aibu kufanya kazi hiyo na wengi wanampongeza na kumtia moyo maana amekuwa Mwanamke wa tofauti. Amewaasa Wanawake wenzake wasichague kazi.
Namba ya kumsupport Zuwena ni hii 0624638385 (Jina la Usajili WALEN GEORGE).
MKE ATOROKA NYUMBANI HAJULIKANI ALIPO, MUME AFUNGUKA “KANIACHIA WATOTO, MKWE ANAPINDISHA MANENO”