Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha Wanamaji cha Marekani.
Ameandika historia kwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na Wanamaji na atatunukiwa cheo cha ‘Wings of Gold’ au ‘mbawa za dhahabu’ baadae mwezi huu wa July, kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa na Mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi.
BZ to Lt. j.g. Madeline Swegle on completing the Tactical Air (Strike) aviator syllabus. Swegle is the @USNavy’s first known Black female TACAIR pilot and will receive her Wings of Gold later this month. HOOYAH! @FlyNavy @NASKPAO #ForgedByTheSea #CNATRA #CNATRAgrads pic.twitter.com/FKSlURWQhJ
— Naval Air Training (@CNATRA) July 9, 2020
Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi alimsifu Swegle akitumia herufi ‘BZ’ au “Bravo Zulu” neno linalotumiwa na Wanajeshi Wanamaji lenye maana “umefanya vyema”.
“BZ kwa Lt. J.G. Madeline Swegle kwa kumaliza mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi (ya mashambulio) ya anga” Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi ya ndege za kivita za majini.
Swegle ni Mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anayetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea Mbawa za dhahabu baadae mwezi huu .
Kwa mujibu wa Jeshi la Majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kumhusu rubani huyu mpya, Swegle kwa sasa yuko katika kituo cha mafunzi cha Redhawks Squadron (VT) 21 katika kituo cha ndege za vita za wanamaji Naval Air Station cha Kingsville kilichopo Texas.
MAFURIKO: MASTAA NA WATU MAARUFU WALIOCHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE 2020