Uamuzi wa mwanamke mwenye umri wa miaka 40 kuacha kazi yake na kuwa ‘binti wa kudumu’ katika kuajiriwa na wazazi wake mwenyewe umezua utata nchini China.
Mwaka jana, baada ya miaka 15 ya kufanya kazi katika shirika la habari, Nianan mwenye umri wa miaka 40 aliacha kazi yake.
Alilazimika kuwa kwenye simu takribani saa 24 kwa siku na kila mara alikuwa mtu mwenye stress Saną na kwa bahati nzuri, wazazi wake walikuja na ofa bora zaidi ya kuajiriwa ikiwa tu angeacha kazi ambayo ilimsumbua sana.
“Kwa nini usiache tu kazi yako? Tutakutunza kifedha,” wazazi wa mwanamke huyo walisema, na kuahidi kumlipa yuan 4,000 sawa na zaidi ya tsh milion 1 laki 3 na 48 kila mwezi ikiwa angekuja tu na kuishi nao.
Baada ya kuajiriwa na wazazi wake ilimaanisha kutokuwepo tena kwa gharama za nyumba, na kuokoa sana gharama za chakula na vitu mbalimbali vya nyumbani, kwani wazazi walishughulikia gharama hizo kwa hiyo Nianan aliacha kazi yake na kuwa mtoto wa nyumbani.
Baada ya mwaka mmoja katika kazi ya wazazi wake, Nianan anaelezea taaluma yake kama “iliyojaa upendo” huku majukumu yake yakiwa ni kupika chakula cha jioni nao , huwatembeza wanapokuwa wanahitaji, na hata ana wakati kucheza nao kila siku,kusimamia vifaa vya elektroniki karibu na nyumba, na kupanga safari moja au mbili za familia kila mwezi.
Ingawa utaratibu huu unaweza kuonekana kuwa wa kufurahisha, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 anasema kwamba bado wakati mwingine anahisi “hamu ya kupata pesa zaidi”. Kwa bahati nzuri, wazazi wake hawana chochote dhidi ya hilo, ikiwa ni kile anachotaka.
“Ukipata kazi inayofaa zaidi, unaweza kuitafuta,” wazazi wa Nianan walimwambia. “Ikiwa hutaki kufanya kazi, kaa tu nyumbani na utumie wakati nasi.”
Nianan aliliambia gazeti la South China Morning Post kwamba mshahara wake wa kila mwezi hulipwa kutoka kwenye pensheni ya kila mwezi ya wazazi wake ya karibu yuan 100,000 sawa na zaidi ya Tsh 35,475,000.
Mpangilio huu usio wa kawaida ulizua mjadala mkali mtandaoni nchini Uchina wiki hii, huku baadhi ya watu wakimkosoa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa kuishi kwa kutegemea wazazi wake, na wengine wakidai kuwa hiyo ilikuwa biashara yao tu kama familia.