Hilde Dosogne mwenye umri wa miaka 55 wa Ubelgiji hivi majuzi aliweka rekodi mpya ya dunia baada ya kushiriki mbio nyingi na mfululizo hii ni baada ya kukimbia marathoni kamili 366 (zaidi ya kilomita 15,000) mnamo 2024.
Mnamo Mei 30, 2024, Hilde Dosogne alikuwa tayari amevunja rekodi ya dunia ya wanawake kwa kufanya marathoni nyingi zilizofikia 150, iliyowekwa na Erchana Murray Bartlett – lakini hakuacha kukimbia hadi Desemba 31, aliporekodi mbio zake za marathon za 366 mfululizo za mwaka 2024.
Ni mafanikio makubwa sambamba na yale ya kitengo cha wanaume yaliyowekwa mwaka wa 2023 na mwanariadha wa Brazil Hugo Farias ambaye pia alikamilisha mbio za marathoni 366.
Kama unavyoweza kufikiria, kukimbia kilomita 42.195 kwa siku, kila siku, kwa mwaka ni kazi kubwa kwa mwili, lakini Hilde alilazimika kuushinda uchovu na kuvimba kwa viungo)
“Kiakili, niliidharau,” Hilde alisema kuhusu changamoto hiyo. “Ni ngumu zaidi kujiandaa kwa hilo. Nilianza kila mbio za marathoni kwa wakati uliokubaliwa ili watu wajue kila wakati wangeweza kujiunga nami kukimbia.
Unapaswa kuwa huko kila wakati: gizani, kwenye baridi, mvua, unakimbia tu.
Hilde alimaliza mbio zake nyingi za marathoni kuzunguka Watersportbaan, uwanja mkubwa wa mafunzo ya kupiga makasia huko Ghent, akikimbia mizunguko 8 ya kilomita 5 kila wakati, na ziada ya kilomita 2.5 kufikia kilomita 42.195.
Kwa mazoezi, kila mara alikimbia hadi saa yake ya GPS ilionyesha kilomita 42.5, ili tu kuwa na uhakika.
Inakadiriwa kuwa mwanamke huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 55 alikimbia angalau mizunguko 2,000 kuzunguka Watersportbaan mwaka jana.