Mwanamume aliyeua watu 35 kwa kugonga umati wa watu katika kituo cha michezo kusini mwa China amehukumiwa kifo, vyombo vya habari vya serikali viliripoti Ijumaa.
Fan Weiqiu, mwenye umri wa miaka 62, aliligonga kwa gari lake watu waliokuwa wakifanya mazoezi kwenye ukumbi wa nje katika mji wa Zhuhai mwezi uliopita, ikiwa ni kitendo cha kutisha cha ukatili dhidi ya umma katika muongo mmoja uliopita.
China imekumbwa na ongezeko la matukio ya ghasia ya ghafla yanayowalenga watu wa kawaida – wakiwemo watoto – katika miezi ya hivi karibuni huku uchumi ukidorora, na kuwatia wasiwasi umma uliozoea viwango vya chini vya uhalifu kwa muda mrefu na ufuatiliaji wa kila mahali