Habari za Mastaa

Mwanamuziki afariki Dunia baada ya kuugua Corona

on

Mwanamuziki, mwandishi na mpuliza saxophone maarufu Duniani Emanuel N’Djoke Dibango ( MANU DIBANGO) mzaliwa wa Cameroon amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 86 kwa Ugonjwa wa Virusi vya Corona.

 

Man Dibango alikuwa akiishi Ufaransa na moja kati ya visa vya kukumbukwa ni pale marehemu Manu Dibango alipodai hakimiliki kutoka kwa gwiji wa Pop duniani Michael Jackson kwa kutumia vionjo vya SOUL MAKOSSA ya Dibango katika wimbo wa Wanna Be Startin’ Somethin’ wa Michael Jackson.

Dibango alitamba sana katika upulizaji saxophone, muziki wa Jazz, uandishi wa nyimbo na hata kuchanganya vionjo vya asili toka Cameroon na kuvipaza katika majukwaa ya kimataifa Duniani.

Dibango ameacha watoto watatu
Georgia Dibango, Marva Dibango, Michael Dibango.

R.I.P DIBANGO.

 

ISIKUPITE HII YA WOLPER KUINGIA WOGA BAADA YA WANAUME KUJITOKEZA KUMZALISHA WATOTO

Soma na hizi

Tupia Comments