Michezo

Huyu ndiye mwanariadha aliyefariki kwa ajali

on

MulaMbulaine Mulaudzi ambaye alikuwa mwanariadha mahiri nchini Afrika Kusini amefariki kwa ajali akiwa safarini kuelekea Johannesburg kushiriki kikao cha wanariadha.

Rais wa chama cha kimataifa cha riadha (IOC) Thomas Bach amesema Mulaudzi alikuwa mwanariadha wa pekee ambapo anatajwa kuwa mmoja ya wanariadha na wanamichezo ambao Afrika Kusini itaendelea kuwaenzi kwa mchango mkubwa alioufanya kuiinua nchi hiyo katika ramani ya michezo. .

Mulaudzi amewahi kushinda medali mbali mbali kama inavyooneshwa hapa:-

2002 –Alishinda medali ya Dhahabu mashindano ya jumuia ya madola

2003 –Alishinda medali ya Shaba

2004 –Alishinda medali ya Dhahabu mashindano ya michezo ya ndani

2006 –Alishinda medali ya Fedha mashindano ya michezo ya ndani

2008 –Alishinda medali ya Fedha mashindano ya michezo ya ndani

2009 –Alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia ya mita 800

Mulaudzi alitangaza kustaafu riadha mwaka 2013, japo aliendelea kujihusisha na masuala ya riadha mpaka kipindi ambacho amefikwa na umauti saa chache zilizopita.

 

 

Tupia Comments