Moja kati ya story iliyoshika hisia za wakazi wengi ni juu ya mwanaume aitwae Randy Cox, kutoka Connecticut, ambaye alifikia makubaliano ya dola milioni 45 na jiji la New Haven baada ya kupooza ndani ya gari la polisi kwa ajali ya bahati mbaya.
Cox alikamatwa mwaka jana na kuwekwa kwenye gari la uchukuzi la polisi akiwa amefungwa pingu ,wakati wa safari hiyo, alipata jeraha la uti wa mgongo lililomfanya kupooza kuanzia shingoni kwenda chini na tukio hilo lilitokea ambapo dereva wa gari la polisi alishika breki ghafla na kupata ajali iliyosababisha Cox kurushwa mbele,kugonga kichwa chake kwenye chuma na kudondoka chini.
Fidia hiyo ni mojawapo malipo makubwa zaidi kuwahi kulipwa na jiji la New Haven na yanalenga kufidia Cox kwa uharibifu alioupata kutokana na tukio hilo.
Wakili wa Cox, David Rosen, alisema suluhu hiyo ilifikiwa baada ya miaka mingi ya mashauriano na mazungumzo na jiji hilo.
Rosen pia alisisitiza kuwa suluhu hii inatumika kama ukumbusho kwamba maafisa wa polisi lazima wawajibishwe kwa matendo yao na kwamba waathiriwa wa ukatili wa polisi wanastahili haki. Tukio hilo linalomhusisha Randy Cox linaangazia suala la ukatili wa polisi na matumizi ya nguvu kupita kiasi nchini Marekani.
Ina semekana kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na visa vingi ambapo watu wamejeruhiwa au kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi huku maandamano ya Black Lives Matter yakionekana kuleta uangalizi zaidi kwa masuala ya unyanyasaji hsa wa rangi na limetoa wito wa marekebisho katika mazoea ya kutekeleza sheria.
Maoni ya wengi yalionyesha kuwa upatikanaji wa suluhu ya Cox inatuma ujumbe kwamba maafisa wa polisi lazima wawajibike kwa matendo yao na kwamba waathiriwa wa ukatili wa polisi wanastahili haki na fidia.