Joseph Moulton, 36, alizunguka kituo cha Polisi cha Naples kwa takriban dakika 40 Jumamosi iliyopita. Luteni wa Polisi wa Naples Bryan McGinn aliambia toleo la Ndani kwamba idara hiyo huwa na wafanyakazi wachache wakati wa saa za jioni, kwa hivyo wasafirishaji na maafisa wengine katika ofisi tofauti hawakumwona akiingia kwenye jengo hilo.
Kulingana na McGinn, inasemekana mshukiwa aliiweza kuvunja mlango na kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo cha wanaume ambako alioga, akatembea kuzunguka kwenye corridor ndani ya kituo akiwa na taulo tu, akajisaidia haja kubwa kwenye ghorofa ya chumba cha kubadilishia nguo cha wanawake, na kuiba koti la kuzuia risasi [bullet proof] kabla ya kuchukua sare nyingine na kisha kutupa redio ya polisi kwenye choo na kurudi nje.
Moulton aliondoka mwendo wa saa 12:39 asubuhi, lakini afisa ambaye aliingia kituoni mwendo wa saa 2 asubuhi alisema waligundua begi la mazoezi kwenye meza kwenye chumba cha mapumziko na baadaye walipata mkoba wake kwenye gari la doria na kuanza upekuzi wao huku picha za usalama zikionyesha matukio ya Moulton kuzunguka kwenye jen hilo.
Moulton alionekana mara ya mwisho mwendo wa saa 1 asubuhi akiwa amevalia sare za polisi, lakini alikamatwa mwendo wa saa 6 asubuhi na alishtakiwa kwa makosa ya wizi lakini baadaye aliachiliwa kwa dhamana ya $30,000 na anatarajiwa kufika mahakamani Mei 1 na mpaka sasa hajawasilisha ombi lolote.