Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Good News kutoka kwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhusu Mikopo kwa wakulima

on

Leo June 12, 2018 Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa amewataka wakulima wa mboga na matunda kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopesheka na Benki ya Kilimo.

Dr. Mwanjelwa anatoa kauli hii akiwa Mkoani Iringa akiwa ameambatana na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji ambayo imetembelea mashamba ya wakulima wa Mboga na matunda ambao wana maghala ya kuhifadhia na kufungasha bidhaa hizo.

Katika ziara hiyo Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji wameshauri , wakati mwingine inapofanyika ziara kama hiyo Wizara ya Kilimo ihakikisha wataalamu wa Kilimo na Maafisa wa Benki wanakuwepo ili kusaidia kutatua changamoto ambazo zinaulizwa na wakulima.

Soma na hizi

Tupia Comments