Baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuibadilisha ZRB ambayo ilikuwa ni Bodi ya Mapato Zanzibar na kuwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Kamishna Mkuu wa ZRA Yusuph Juma Mwenda amezindua rasmi nembo ya ZRA na kuanza kutumika.
“Niwashukuru Wabunifu wote ambao jumla yao ni 60, katika Wabunifu 60 walioleta nembo 62 ni Watu wengi wamejitokeza, nembo hii inawakilisha Mamlaka hii, nembo ina saini kubwa kwetu tunaizindua na tunaanza kuitumia na tunaitumia kwa ujumbe wa kwamba hatutamuonea Mtu, hatutamuonea Mlipa kodi na hatutompendelea Mlipa kodi”