Kihage ameyasema hayo Jijini Dar es salaam leo wakati akieleza mwenendo wa bei za bidhaa muhimu nchini kwa mwezi December 2022 na kusema kuwa mfumuko wa bei nchini Tanzania ni wa kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na nchi jirani ambapo Tanzania mfumuko wa bei kwa mwezi November ni asilimia 4.9, Kenya asilimia 7.38, Uganda asilimia 10.6 na Rwanda asilimia 21.7.
Bei ya mchele kwa mwezi December ni kati ya Shilingi 2,200 na 3,500 kwa kilo, bei ya chini na ya juu imepanda kutoka 2,000 na 3,200 kwa kulinganisha na mwezi November, Mikoa yenye bei ya chini ni Katavi na Ruvuma na bei ya juu ipo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Manyara na Arusha.
Bei ya unga wa ngano kwa mwezi Desemba ni kati ya Shilingi 2,000 na 2,500 kwa kilo, bei ya unga wa ngano imeonesha uhimilivu ikilinganishwa na mwezi Novemba, bei ya juu ipo katika Mikoa ya Manyara, Rukwa na Songwe na bei ya chini ipo katika maeneo mengi nchini.
Bei ya sukari kwa mwezi December ni kati ya Shilingi 2,600 na 3,000 kwa kilo, bei hiyo imeonesha uhimilivu ikilinganishwa na mwezi November, hali hiyo inatokana na jitihada zinazoendelea za kuvutia uwekezaji na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa sukari nchini.