Paul Makonda, Katibu wa NEC itikadi,uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi amesema atapendekeza kutolipwa mishahara kwa watendaji wa serikali ambao wamekuwa wazembe katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwenezi Makonda ametoa kauli hiyo Sumbawanga vijijini kwenye kata ya Miangulia baada ya kukuta malalamiko ya wananchi wanaodai kutokujengwa kwa barabara ya Kavifuti kwenda Miangalua licha ya benki ya dunia kutoa fedha za mradi huo wakati wa bajeti ya mwaka 2022/23.
Mwenezi Makonda wakati akizungumza na Meneja wa Tarura wa eneo hilo amesema uzembe wa kutokukamilisha miradi kwa wakati umekuwa ukikigharimu Chama Cha Mapinduzi kutokana na kushindwa kukamilisha ahadi walizoziahidi kwa wananchi.
Kulingana na wananchi, Benki ya dunia ilitoa Milioni 352 kwenye mwaka wa fedha 2022/23 na kufikia leo Tarura inasema inaendelea na mchakato wa manunuzi kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo.