Mwenye nyumba kaskazini mwa Ufaransa amewaacha wanamitandao kwenye mshangao baada ya kujaribu kuwalazimisha wapangaji wake kuondoka katikati ya msimu wa baridi kwa kuondoa milango na madirisha kwenye nyumba yake aliowapangishia
Nchini Ufaransa, kama ilivyo katika nchi nyingi za Ulaya, ni kinyume cha sheria kuwafukuza wapangaji wakati wa majira ya baridi kali, hata kama hawajalipa kodi licha ya sheria hiyo mwenye nyumba huyo,kaskazini mwa Ufaransa, alijariburibu kukiuka sheria kwa kuwalazimisha wapangaji wake kuondoka kwenye nyumba hiyo mara moja
Mnamo Desemba 20, timu ya wafanyikazi walilifika katika eneo hilo na kuanza kung’oa milango na madirisha kwa kisingizio cha kuyabadilisha.
Hata hivyo, wapangaji hao wanadai kuwa walipakia tu milango na madirisha ya zamani kwenye gari na kuondoka na kuwaacha wakikabiliana na baridi kali saa zote za mchana na usiku.