Top Stories

Mwenyekiti aomba kibali cha kukamatwa kwa Mbunge Jerry Silaa (video)

on

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili na madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka aomba kibali cha Spika wa Bunge kukamatwa kwa Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa na kupelekwa mbele ya kamati kesho saa nne kutokana na kutofika mbele ya kamati leo saa tano kama ilivyokuwa imepangwa.

Mwakasaka amesema kuwa Mbunge Jerry Silaa hakutoa taarifa za kutofika kwake na kwamba kamati imemsubiri hadi saa 8.00 mchana lakini hakutokea hivyo wamemwomba Spika kutoa kibali cha kukamatwa kwake na kufikishwa katika kikao cha kamati.

Itakumbukwa Jerry Silaa alifika Bungeni August 24,2021 kuitikia wito uliomtaka kufika mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge ambapo baada ya mahojiano alitakiwa arudi tena leo ili kuendelea kuhojiwa.

MBUNGE JERRY AFUNGUKA BAADA YA MAHOJIANO NA KAMATI/ ISHU YA KUKATAA KUSINDIKIZWA NA ASKARI AJIBU

Soma na hizi

Tupia Comments