Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido, Simon Oitesoi ameingia kwenye mgogoro wa kiuongozi na kutakiwa kujiuzulu kufuatia kushindwa kusimamia Mamlaka yake ipasavyo katika Baraza la Madiwani na kuruhusu upotevu wa mamilioni ya pesa za Halmashauri hiyo kunakofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.
Katika kikao kilichoketi cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Mwenyekiti huyo alionekana kuwa busy na simu wakati kikao kikiendelea jambo linalotazamwa kama ni utovu wa nidhamu kwa Mkuu wa wWlaya MARKO NG’UMBI aliyekuwa akitoa maelekezo ya serikali.
Baadhi ya madiwani walidai kuwa ulegevu wa Mwenyekiti umelikosesha meno baraza hilo kiasi cha kushindwa kuhoji matumizi mabaya ya fedha yanayosababishwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo.
Katika baraza hilo mkuu wa wilaya alilieleza baraza hilo la madiwani jinsi baraza hilo limeshindwa kusimamia mapato ya halmashauri huku fedha nyingi zikipotea bila kuwepo usimamizi .
Alisema makusanyo ya halmashauri hadi desemba mwaka jana yalifikia zaidi ya bilioni 1.036 lakini hadi sasa ni sh,milioni 90 pekee zimeenda kwenye maendeleo na hiyo ni chini ya asilimia 7 tu ambayo ni kinyume na utaratibu unaozitaka halmashauri kutoa asilimia 40 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti huyo, Simon Oitesoi alipohojiwa kwa njia ya simu alidai kwamba yeye sio legevu kama anavyozushiwa ila amefanya jitihada kubwa kupitia kamati ya fedha na baraza la madiwa kusimamishwa kwa viongozi sita wa halmashauri hiyo na kwamba hana taarifa za yeye kujiuzulu na kwamba hayuko tayari kujiuzulu
Baadhi ya vijana kutoka wilaya hiyo ya Longido wamezungumza na vyombo vya habari nakuiomba serikali kuunda tume maalumu itakakayochunguza Halmashauri hiyo