Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Mwenyekiti Halmashauri Longido atakiwa kujiuzulu
Share
Notification Show More
Latest News
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo May 30, 2023
May 30, 2023
Waziri Masauni asimama Bungeni Mei 29, 2023 ‘Watanzania 66 waukana Uraia’
May 29, 2023
Sentensi za Mkurugenzi wa Asas kwenye Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT)
May 29, 2023
Hospitali yachunguzwa kwa madai ya kuwaweka watoto wachanga kwenye maboksi
May 29, 2023
Marekani yabatilisha visa ya spika wa bunge la Uganda baada ya saini Mswada mkali wa ushoga kuwa sheria
May 29, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Mwenyekiti Halmashauri Longido atakiwa kujiuzulu
Top Stories

Mwenyekiti Halmashauri Longido atakiwa kujiuzulu

February 28, 2023
Share
2 Min Read
SHARE

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido, Simon Oitesoi ameingia kwenye mgogoro wa kiuongozi na kutakiwa kujiuzulu kufuatia kushindwa kusimamia Mamlaka yake ipasavyo katika Baraza la Madiwani na kuruhusu upotevu wa mamilioni ya pesa za Halmashauri hiyo kunakofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

Katika kikao kilichoketi cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Mwenyekiti huyo alionekana kuwa busy na simu wakati kikao kikiendelea jambo linalotazamwa kama ni utovu wa nidhamu kwa Mkuu wa wWlaya MARKO NG’UMBI aliyekuwa akitoa maelekezo ya serikali.

Baadhi ya madiwani walidai kuwa ulegevu wa Mwenyekiti umelikosesha meno baraza hilo kiasi cha kushindwa kuhoji matumizi mabaya ya fedha yanayosababishwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo.

Katika baraza hilo mkuu wa wilaya alilieleza baraza hilo la madiwani jinsi baraza hilo limeshindwa kusimamia mapato ya halmashauri huku fedha nyingi zikipotea bila kuwepo usimamizi .

Alisema makusanyo ya halmashauri hadi desemba mwaka jana yalifikia zaidi ya bilioni 1.036 lakini hadi sasa ni sh,milioni 90 pekee zimeenda kwenye maendeleo na hiyo ni chini ya asilimia 7 tu ambayo ni kinyume na utaratibu unaozitaka halmashauri kutoa asilimia 40 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo, Simon Oitesoi alipohojiwa kwa njia ya simu alidai kwamba yeye sio legevu kama anavyozushiwa ila amefanya jitihada kubwa kupitia kamati ya fedha na baraza la madiwa kusimamishwa kwa viongozi sita wa halmashauri hiyo na kwamba hana taarifa za yeye kujiuzulu na kwamba hayuko tayari kujiuzulu

Baadhi ya vijana kutoka wilaya hiyo ya Longido wamezungumza na vyombo vya habari nakuiomba serikali kuunda tume maalumu itakakayochunguza Halmashauri hiyo

You Might Also Like

Waziri Masauni asimama Bungeni Mei 29, 2023 ‘Watanzania 66 waukana Uraia’

Sentensi za Mkurugenzi wa Asas kwenye Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT)

Hospitali yachunguzwa kwa madai ya kuwaweka watoto wachanga kwenye maboksi

Marekani yabatilisha visa ya spika wa bunge la Uganda baada ya saini Mswada mkali wa ushoga kuwa sheria

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov azuru Kenya

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA February 28, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 28, 2023
Next Article Wakwe na Mume wafanya mauaji na kuficha sehemu za mwili kwenye friji!
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo May 30, 2023
Magazeti May 30, 2023
Waziri Masauni asimama Bungeni Mei 29, 2023 ‘Watanzania 66 waukana Uraia’
Top Stories May 29, 2023
Sentensi za Mkurugenzi wa Asas kwenye Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT)
Top Stories May 29, 2023
Hospitali yachunguzwa kwa madai ya kuwaweka watoto wachanga kwenye maboksi
Top Stories May 29, 2023

You Might also Like

Top Stories

Waziri Masauni asimama Bungeni Mei 29, 2023 ‘Watanzania 66 waukana Uraia’

May 29, 2023
Top Stories

Sentensi za Mkurugenzi wa Asas kwenye Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT)

May 29, 2023

Marekani yabatilisha visa ya spika wa bunge la Uganda baada ya saini Mswada mkali wa ushoga kuwa sheria

May 29, 2023
Top Stories

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov azuru Kenya

May 29, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?