Mwenyekiti wa Chama cha Mama lishe “Mama ntilie” Tanzania UMALIKIDA Avijawa omari amegawa Mitungi ya Gesi kwa Mama ntilie zaidi ya 10 lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.
Mwenyekiti huyo ambae pia ni mfanyabiashara wa mgahawa amekabidhi mitungi hiyo mbele ya Bi Agusta Safale ambae alifika kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa kwaajili ya tukio hilo na alifika hapo kama muakilishi wa mkuu wa wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo.
Mwenyekiti Avijawa amesema , Amefanya hivyo kuunga mkono jitihada za Mhe Rais za matumizi ya nishati safi lakini pia kukomboa maisha ya Mamalishe “Mama ntilie” hao ambao kimsingi aliwakuta katika hali ambazo hazilishi na kupelekea kupata changamoto za biashara zao.
Kwa upande wake muakilishi wa mgeni rasmi Bi Agusta amesema sio tu wakina Mama wajitokeze kuunga mkono jitihada hizi za Mhe.Rais bali pia watu wote ili kunusuru mazingira ya nchi yetu na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi.
Hatahivyo sio Mitungi ya gesi pekee Mamalishe hao wamepokea pia vifaa vya jikoni kadhaa ikiwemo Masufuria, na vifaa vingine vitakavyotumiwa katika mapishi.
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alizindua mkakati wa taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2033 mapema mwaka huu 2024 wakati aliposhiriki Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) huko Dubai.