Mwenjekiti mpya wa Chama cha soka Wilaya ya Temeke (TEFA)amemteua Alexander Luambano kuwa Makamu Mwenyezi wake na hii ni kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo February 7,2025,Jijini Dar Es Salaam.
Luambano amehudumu kwa takribani miaka minne kama Makamu Mwenyekiti wa pili wa TEFA na sasa anakua Makamu Mwenyekiti wa wa kwanza wa Chama hicho.
Mtangangazaji huyo nguli wa Michezo nchini,amepewa nafasi hiyo ikiaminika kuwa atakua na msaada mkubwa wa kuusaidia mpira wa Miguu katika Wilaya ya Temeke kupitia taaluma aliyo nayo.
Mapema hii leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Wilaya ya TEMEKE TEFA,Hashim Mziray alimtangaza Mohamed Saleh Mohamed kuwa ndiye Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilayani humo .
Mohamed Saleh Mohamed amepata kura 28 akiwapiku Alexander Luambano aliyepata kura 16 wakati Moalim Milonhea akipata kura 2 katika uchaguzi huo.
Jumla ya wapiga kura 48 kati ya 70 waliohudhuria mkutano huo Mkuu wa Uchaguzi wa TEFA ambao hapo awali ulikumbwa na hekaheka za kufutwa kutokana na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi.
Katika nafasi ya utendaji wa Mkutano Mkuu,washindi ni Siza Chinja (kura 43) na Dastan Nchimbi(kura 36) wakiwabwaga Abubakar Magimba(kura 17),Shania Kivumbi (kura 14) na Kazi Ngogota(kura 12).
Nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu washindi ni Thomas Leopard Muhinzi aliyepata kura 36 naye Dibega Ambona akipata kura 12.
Uchaguzi huo umesimamiwa na Mwakilishi kutoka Chama cha soka Dar es salaam,Yusuph Keiwanga ambaye amesema amefurahishwa na zoezi hilo la uchaguzi ambalo limefuata taratibu zote za kikatiba na kikanuni huku akiweka wazi kuwa iwapo kuna mwenye malalamiko juu ya uchaguzi huu ipo nafasi ya kulalamika kupitia nyaraka zenye vielekezo vya kupinga mchakato wa uchaguzi huo.
Mohamed Saleh Mohamed ambaye amekua Makamu Mwenyekiti wa TEFA kwa vipindi vitatu mfululizo anachukua nafasi ya Marehemu Mzee Peter Muhinzi aliyefariki Dunia .