Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida akiwa na Makamu wake Rehema Sombi wamepokelewa Desemba 22, 2022 kwa mara ya kwanza na vijana wa Mkoa wa Dar es salaam.
Hii ikiwa ni baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa UVCCM Novemba 27, 2022 Jijini Dodoma. Vijana wa wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam, wameshiriki katika kumpokea mwenyekiti wa UVCCM wakishirikiana na uongozi wa UVCCM Makao Makuu.
Katika mapokezi hayo makubwa kulikuwa pia na burudani mbalimbali.
Katika mapokezi hayo Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, amewasihi vijana kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, huku akiwaahidi kuwapambani katika nafasi za ajira.
“Wasio elewa hawaelewi lakini sisi waelewa tunaelewa nini umuhimu wa mradi wa bwawa la mwalimu Julias Nyerere, utaende kuondoa adha ya umeme kwa vijana wanao fanya kazi kwa kutegemea umeme”
Kawaida amesema anawashangaa baadhi ya vijana ambao wanasemea vibaya kazi wanayoifanya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kwani miradi hii ndio vijana wanapopata nafsi ya ajira
Pia amewakumbusha vijana wa UVCCM kuvunja makundi, kwani uchaguzi umeisha na sasa ni wakati wa vijana kufanya kazi wakisaidiana na Viongozi wao kuanzia Kata mpaka Taifa.