Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Cde. Mohamed Ali Kawaida ashiriki maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Mkoani Lindi; akiambatanaa na Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa Cde. Rehema Sombi pamoja na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Kenani Kihongosi.
Na Wajumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa- Cde Shamira Mshangama na Cde Gloria Katalambula.
Hili ni tukio la kwanza Kitaifa la Mwneyekiti UVCCM Taifa na Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa- wameanza kazi rasmi- tunawatakia kila la Kheri katika utendaji wao.
Tunawatakia Vijana wote watakaoshiriki kila la Kheri Mkoani Lindi.
Aidha Mwenyekiti wa UVCCM akizungumza na millardayo.com alisema..” Vijana ni deni kwa taifa hivyo mimi kama Mwenyekiti tunaungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hapa Lindi na viongozi mbalimbali katika kuadhimisha siku hii ya Ukimwi Duniani Nawaomba kijana wa kitanzania ni muhimu kupima afya yako kujitambua tujenge taifa letu na kuliletea maendeleo”- Ali Kawaida